Katika video hiyo inayovuma, mwanamume aliyevalia suruali ndefu ananaswa akizungumza na mwanamke wake alipomwacha kwa ghafla na kwenda kwa mwanamume mwingine. READ MORE HERE
Katika harakati hizo walianza kupigana huku yule mwingine akitumia sehemu ya chini ya bunduki kumpiga mwenzake na kumwacha akivuja damu chini.
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linapenda kutoa taarifa kuhusiana na tukio la picha mjongeo (video) zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii tarehe 27.10.2024 zikionyesha mwanaume mmoja akitishia watu kwa silaha.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam lilifuatilia limemkamata na linamshikilia Derick Derick Junior miaka 36, Mkazi wa Salasala Kinondoni kwa tuhuma za Kujeruhi na kutishia kwa silaha, Tukio Hilo baada ya uchunguzi ilibainika lilitokea tarehe 27.10.2024 saa 12.30 asubuhi maeneo ya Masaki ‘1245 night club’ Kinondoni ambapo mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru kwa kumpiga na kitako cha bastola pia kumjeruhi sehemu ya jicho na pua, Kitendo hicho hakikubaliki ni kinyume na sheria aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu
Aidha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika Vyombo vingine vya Sheria haraka iwezekanavyo.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kumchukulia hatau mtu yoyote anayemiliki silaha, atakayebainika kufanya matendo ambayo ni kinyume na Sheria Kanuni na taratibu zilizoainishwa katika kibali chake cha kumiliki silaha.
Imetolewa
Muliro J. Muliro -SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam
28 Oktoba, 2024
www.polisi.go.tz
www.twitter.com/tanpol
www.facebook.com/Polisi.”
VIDEO HERE